Mo awatembelea wachezaji kambini

Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ leo ametembelea kambini na kuzungumza na wachezaji kwa lengo la kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa kesho wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Mo amewakumbusha wachezaji umuhimu wa kushinda mchezo wa kesho sababu mioyo na furaha za Wanasimba zinawategemea hivyo wasiwaangushe.

Mo amewaambia mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Wydad lakini kama watajitoa kwa asilimia 100 na uwepo wa mashabiki wetu uwanjani tutapata ushindi mzuri kesho.

Mo amekuwa na utaratibu wa kutembelea kambini kuzungumza na wachezaji kila tunapokaribia mechi kubwa ili kuwatia hamasa na kuwaongezea morali.

Kutokana na ukubwa na umuhimu wa mchezo Mo ameambatana na Bodi ya Wakurugenzi ili kuwasisitiza wachezaji kujitoa kuhakikisha ushindi unapatikana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER