Mo awaeleza wachezaji nia yake Kombe la Afrika

 

Rais wa Heshima na Mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’ amewaeleza wachezaji kuwa nia yake ni siku moja kuiona tunafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mo ameyasema hayo baada ya kutembelea kambi Mjini Dubai ambapo amewaambia wachezaji kila kitu kinawezekana kama watafanya jitihada kwenye mechi zetu.

Kabla ya kufika hatua ya kuchukua ubingwa wa Afrika, Mo amewataka wachezaji wapambane kuhakikisha tunarejesha ubingwa wa ligi na Kombe la Shirikisho la Azam ambao msimu uliopita tuliupoteza.

“Siku zote dhamira yangu ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa Kombe la Afrika na hilo linawezekana kama tukiweka nia.

“Kabla ya yote kwanza tuanze na kurejesha ubingwa wetu wa ligi pamoja na Kombe la FA hilo ndilo kubwa, imani yangu ni kuwa kila kitu kinawezekana kama tukiweka jitihada,” amesema Mo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER