Mo Assurance yaingia mkataba wa bima ya afya na Klabu

Kampuni ya Bima ya Mo Assurance imeingia mkataba wa miaka miwili ya kugharamia huduma za afya kwa wafanyakazi wote wa klabu sanjari na kutoa kitita cha Sh milioni 250 kwa mwaka.

Mo Assurance itagharamia huduma ya afya kwa wafanyakazi wote wa klabu, wachezaji wa timu ya wanaume, Simba Queens, timu ya vijana utakaohusisha wategemezi wanne kutoka kwenye familia zao.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema Mo Assurance itagharamia matibabu kwa asilimia 100 pamoja na kutoa kiasi hicho cha pesa kwa mwaka.

“Leo tumeingia historia mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Bima ya Mo Assurance ambapo wafanyakazi wote wa Simba pamoja na wategemezi wao wanne watagharamiwa huduma za matibabu,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mo Assurance Gregory Fortes amesema bima hiyo itawafanya wachezaji kutokuwa na wasiwasi kuhusu afya zao na wataweka akili zao uwanjani zaidi na kuipa mafanikio timu.

“Hii itawafanya wachezaji kutokuwa na wasiwasi wa afya zao pamoja na watu wanne wa familia, wataweka akili zao uwanjani zaidi na itakuwa faida kwa timu,” amesema Fortes.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER