Mo ashusha viingilio vya mchezo dhidi ya Raja Casablanca

Rais wa Heshima na muwekazaji wa klabu, Mohamed Dewji ameagiza kushushwa kwa viingilio vya mchezo wetu wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Jumamosi Februari 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Awali kiingilio cha chini ambapo ni mzunguko kilikuwa Sh. 5000 lakini sasa itakuwa Sh. 3000 wakati VIP C ilikuwa 20,000 ila kwa sasa itakuwa Sh. 10,000.

Mo amechukua maamuzi hayo ili kuwafanya mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ili tufanye.

Viingilio vipya vilivyopangwa

Mzunguko Sh. 3,000
VIP C Sh. 10,000
VIP B Sh. 20,000
VIP A Sh. 30,000

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao muda mfupi ujao tutatangaza vituo ambavyo zitapatikana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER