Rais wa heshima ambaye pia ni mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’ amemteua Salim Abdallah ‘Try Again’ kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba.
Mo alimteua Try Again kuchukua nafasi yake Septemba mwaka 2021 baada kubanwa na shughuli zake za biashara ambapo amefanya kazi nzuri kabla ya kumteua tena.
Mo amesema ana imani na Try Again kuwa ataingoza Simba kufikia mafanikio makubwa zaidi barani Afrika na duniani kwa ujumla.
“Umefanya kazi nzuri nina imani na wewe. Nategemea utaifikisha Simba kwenye mafanikio makubwa ya soka barani Afrika na duniani kwa ujumla,” amesema Mo.