Mo amkaribisha Robertinho, amuahidi ushirikiano mkubwa

 

Rais wa Heshima wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amemkaribisha Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ambapo amemuahidi kumpa ushirikiano mkubwa.

Baada ya kuitembelea kambi Mjini Dubai Mo amemuahidi Kocha Robertinho kuwa katika dirisha hili la usajili atamuongezea wachezaji wengine wazuri ili aweze kutimiza malengo yake na klabu.

“Binafsi nakukaribisha sana Simba, tunaamini uzoefu wako na dhamira yako kwa timu, sisi tutakupa ushirikiano mkubwa na tutakuongezea wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili ili uifanye kazi yako kwa usahihi,” amesema Mo.

Katika mazungumzo yake na benchi la ufundi Mo amempongeza na kumshkuru Kocha Juma Mgunda kwa kukubali kuichukua timu katika nyakati ngumu na ameweza kuifanya kuwa imara zaidi.

Katika hatua nyingine Mo amewashukuru wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wanaomaliza muda wao na amewatakia heri wanachama kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 29.

“Namshukuru Afisa Mtendaj Mkuu wetu, Barbara Gonzalez kwa kazi nzuri aliyoifanya naaamini ataendelea kuwa Simba na sisi tutaendelea kumpa ushirikiano,” amesema Mo.

Mwisho kabisa Mo amewataka wachezaji kutosikiliza maneno ya watu kuhusu yeye na kwani bado yupo sana na anawapenda na anaipenda mno Simba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER