Mo aipigia ‘saluti’ Queens

Rais wa Heshima wa Klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameipongeza Simba Queens kwa kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika upande wa Wanawake.

Mo amesema Queens imetuheshimisha na kuendelea kuitangaza Simba kimataifa jambo ambalo ndiyo malengo tuliyojiwekea kwa ajili ya mafanikio ya klabu.

“Hongereni sana Simba Queens kwa kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Afrika kwa mara ya kwanza katika historia. Mmetufanya tujivunie sana. Nusu Fainali tunakuja,” amesema Mo.

Aidha, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pia limeipongeza Simba Queens kwa hatua hiyo kutokana na kuendelea kuipeperusha vema 1bendera ya nchi.

Queens imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Green Buffaloes na kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi A.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER