Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kabla ya mchezo kulikuwa na maneno mengi ya kuchagiza nje ya uwanja kama ilivyo kawaida ya mechi za Derby ya Kariakoo lakini mwisho wa siku sisi ndio washindi.
Tulianza mchezo kwa kasi ambapo tulipata bao la kwanza dakika ya kwanza kwa kichwa kupitia kwa mlinzi wa kati Henock Inonga akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.
Kibu Denis alitupatia bao la pili kwa shuti kali nje kidogo ya 18 dakika ya 31 baada ya kumpoka mpira Bakari Mwamnyeto.
Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi na kutafuta bao lakini tulitulia na kuhakikisha hatufanyi makosa ambayo yangeweza kutugharimu.
X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Henock, Erasto (Kapama 73′), Chama, Mzamiru, Baleke (Bocco 82′), Ntibazonkiza, Kibu.
Walionyeshwa kadi: Kibu 29′ Ally 69′
X1: Diarra, Djuma, Lomalisa, Mwamnyeto, Job, Aucho, Moloko (Tuisila 45′), Bangala (Mudathir 45′) Mayele, Sure Boy (Azizi Ki 45′), Musonda (Morrison 70′)
Walionyeshwa kadi: Djuma 55′