MNYAMA MAWINDONI TENA LEO KUWAVAA JKT TANZANIA

Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili Maafande wa JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambayo tumeingia mzunguko wa pili.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza tuliocheza kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma tuliibuka na ushindi wa mabao 4-0 yaliyofungwa na Medie Kagere aliyefunga mawili, Chris Mugalu na Luis Miquissone.

Kikosi kinaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya African Lyon siku ya Ijumaa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mratibu wa timu, Abbas Ally amesema kikosi kipo kamili na wachezaji wote 28 wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa mchezo na kumpa wigo mpana kocha Didier Gomez kuchagua nyota 18 watakaonza.

“Kikosi kipo kamili na hakuna mchezaji majeruhi kwahiyo benchi la ufundi litaamua nani aanze nani akae benchi lakini kiujumla tuko tayari kwa mchezo,” amesema Abbas.

Mpaka sasa tupo nafasi ya pili kwenye msimamo tukiwa na alama 42 baada ya kucheza mechi 18 tukiwa na mechi tatu mkononi kulinganisha na wanaongoza Ligi.

Kama tutapata ushindi leo tutafikisha alama 45 pointi nne nyuma ya wanaongoza huku tukiwa na mechi mbili mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Nawaomba wachezaji wasidharau mchozo wowote tunaocheza maana tunahitaji mataji yote tunayoshiriki tuyachukue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER