Mkude, Morrison kuanza dhidi ya Vita leo

Kiungo mkabaji, Jonas Mkude na Winga Bernard Morrison leo wamepangwa kuanza kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani kuikabili AS Vita kwenye mchezo wa tano hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Mara kadhaa Kocha Didier Gomez amekuwa akimuanzisha Mzamiru Yassin akisaidiana na Taddeo Lwanga kwenye kiungo cha ulinzi lakini leo amepanga kuanza na Mkude.

Kwa upande wa Morrison huwa anatokea benchi akichukua nafasi ya Rally Bwalya akiwa sambamba na Clatous Chama na Luis Miquissone kwenye kiungo cha ushambuliaji.

Kikosi Kamili kilivyopangwa:

 1. Aishi Manula
 2. Shomari Kapombe
 3. Mohamed Hussein
 4. Joash Onyango
 5. Pascal Wawa
 6. Taddeo Lwanga
 7. Bernard Morrison
 8. Jonas Mkude
 9. Chris Mugalu
 10. Clatous Chama
 11. Luis Miquissone

Wachezaji wa Akiba

 1. Beno Kakolanya
 2. Erasto Nyoni
 3. Kennedy Juma
 4. Rally Bwalya
 5. Hassan Dilunga
 6. Medie Kagere
 7. Francis Kahata
SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER