Mkude Mchezaji Bora Desemba

Kiungo mkabaji Jonas Mkude, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Mkude amewashinda walinzi wawili wa kati Joash Onyango na Henock Inonga Baka ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Desemba, Mkude amecheza mechi nne kati ya tano akihusika katika upatikanaji wa mabao mawili (assist) huku akionyesha kiwango bora.

Mkude atakabidhiwa pesa taslimu Sh 2,000,000 pamoja na tuzo kutoka kwa Wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa

Mkude kura 2397 (43.93%)

Onyango kura 2393 (43.85%)

Inonga kura 667 (12.22%)

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Congratulations 👏 to all players for what they do for the advantages of our team,Mungu awalinde.
    HAKIKA 👉🦁💪👉⚽
    SIMBA NGUVU MOJA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER