Mkude, Henock, Onyango wachuana Mchezaji Bora Desemba

Nyota watatu wameingia kwenye fainali ya kinyang’anyiro cha kuwania mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Wachezaji walioingia fainali kutokana na uwezo walioonyesha ni kiungo mkabaji Jonas Mkude, walinzi wakati Henock Inonga na Joash Onyango.

Katika mwezi Desemba, Mkude amecheza mechi nne kati ya tano ambazo amecheza dakika zote 90 huku akisaidia kupatikana kwa mabao mawili (assist) wakati Onyango na Henock wakicheza mechi tatu kila mmoja kwa kiwango cha juu.

Awali walikuwa wachezaji watano pamoja na Kibu Denis na Sadio Kanoute lakini wawili hao wamechujwa na Kamati Maalum ya tuzo na kuwabakisha Mkude, Onyango na Henock.

Zoezi la mashabiki kupiga kura limeanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Januari mosi saa 10 jioni ambapo mwenye kura nyingi atatangazwa mshindi.

Mshindi atakabidhiwa tuzo na pesa taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi.

This poll has ended (since 2 years).
SHARE :
Facebook
Twitter

36 Responses

 1. Mimi ningependa kutoa ushauri. Kwa Pape ousman sakho kua Ligi yetu ni ngumu na Clab nying zna2mia nguvu uwanjan so Ili kuepuka majeruh ya mara kwa mara Asiwe anakaa na mpira mguun mda mref koz wachezaj weng wa bongo wanatumia nguvu kunyang’anya mpira na sio akili
  Mfano mzuri ni majeraha aliyo yapata dhidi ya Dodoma jiji
  Pia kuna team zna2mia nguvu kama Prisons
  Ruvu shooting
  Namungo
  Na nyinginezo
  NB :: ONE TEAM ONE DREAM

 2. Nawapongeza sana Kwa emerate aluminum Kwa tuzo hizi Kwa wachezaji wetu hakika zinawap hamasa ya upambanaji viwanjani.

 3. Tunawaomba viongozi wetu tutumie vizuri dirisha hili dogo kuimarisha timu yetu kwaajili ya confederation cup na ligi.

 4. Ofcouse Jonas mkude I appreciate is the one who makes my heart feels better when Witcher when Nguvu moja playing and for this month makude have made wanderf playing

 5. I would like to appreciate the board of directors, technical bench,fans and team at large for fantastic moves they’re showing to make one the best team….together we succeed divided we fall! @Simbanguvumoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER