Mkude atunyanyua jiooni Sokoine

Bao la dakika za majeruhi lililofungwa na kiungo Jonas Mkude limetuwezesha kuondoka na poiti zote tatu katika Uwanja wa Sokoine baada ya kuifunga Tanzania Prisons.

Mkude alifunga bao hilo dakika ya 85 baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Kibu Denis kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Shomari Kapombe.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambulia kwa nguvu kuhitaji bao la mapema lakini hata hivyo mashambulizi yetu mengi yaliishia kwa walinzi wa Prisons.

Wenyeji Prisons walicheza zaidi soka la kuzuia wakiwa wengi zaidi eneo lao huku wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza ambayo hayakuwa na madhara yoyote kipindi cha kwanza.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Habib Kyombo, Pape Sakho na Henock Inonga na kuwaingiza Kibu Denis, Augustine Okrah, Joash Onyango

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER