Mkataba wa M-Bet ni kufuru

Leo tumetangaza rasmi thamani ya mkataba na mdhamini wetu mkuu Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet wenye thamani ya Sh. Bilioni 26.1 kwa muda wa miaka mitano.

Mkataba huu tulitangaza Julai 14 lakini tulikuwa hatujaweka wazi thamani yake ambaye imevunja rekodi zote ndani ya nchi na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Katika kipindi hicho cha miaka mitano tutakuwa tukipokea pesa katika mchangunuo ufuatao.

Mwaka wa kwanza – Bil 4.670 Mwaka wa pili – Bil 4.925

Mwaka wa tatu – Bil 5.205

Mwaka wa nne – Bil 5.514

Mwaka wa tano – Bil 5.853

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema M-bet wamekidhi mahitaji yetu baada ya majadiliano ya muda mrefu.

Kwa upande waka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewashuku M-bet kwa kuchagua kufanya kazi nasi na kusisitiza hawatajutia.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-bet, Alan Mushi amesema anaamini tutawatangaza vya kutosha sababu tunafanya vizuri na tunashiriki michuano ya kimataifa.

“Simba ni klabu kubwa, kwa miaka minne iliyopita imechukua ubingwa wa ligi mfululizo, sisi tupo kimataifa na Simba inashiriki pia huko kwahiyo tunaamini itatutangaza,” amesema Mushi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER