Miso Misondo apagawisha Mbagala

DJ namba moja kwa sasa nchini, Miso Misondo na kundi lake wameongoza kikosi cha hamasa katika Uwanja wa Zakhem Mbagala kwa ajili ya kuwaita Wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku Jumanne.

Misondo amekuwa gumzo kwa sasa jijini Dar es Salaam na Wakazi wa Mbagala na Viunga vyake wamefurahia burudani safi kutoka huku wakiendelea kununua tiketi za mchezo.

Miso Misondo alikusanya kijiji na kuwafanya mashabiki na wapenzi walijiokeza kulipuka kwa Shangwe muda wote.

Huu ni utaratibu tuliojiwekea kufanya hamasa kuzunguka jiji la Dar es Salaam kuelekea kila mchezo wetu wa nyumbani wa Ligi ya Mabingwa Afrika kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanjani.

Viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh 3000
VIP Sh. 10,000
VIP B Sh. 20,000
VIP A Sh. 30,000
Platinum Sh. 150,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER