Miquissone amerejea unyamani

Tumemsajili kiungo mshambuliaji Jose Luis Miquissone anarejea tena Simba baada ya kuitumikia klabu yetu kwa mafanikio makubwa kabla ya kuuzwa kwa miamba ya Afrika Al Ahly ya Misri miaka miwili iliyopita

Baada ya fununu za muda mrefu hatimae hii leo tumefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji Jose Luis Miquissone raia wa Msumbuji kutoka Al Ahly ya Misri kwa mkataba wa miaka miwili.

Miquissone anarejea tena Simba baada ya kuitumikia klabu yetu kwa mafanikio makubwa kabla ya kuuzwa kwa miamba ya Afrika Al Ahly ya Misri miaka miwili iliyopita

Simba tumemchukua Miquissone kama mchezaji huru baada ya kuvunja Mkataba na klabu yake hiyo.

Kurejea kwa Miquissone ni faida kubwa kwetu kwani tayari ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika lakini kubwa zaidi analijua vema soka la Tanzania.

Tayari Miquissone ameshawasili Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda Uturuki

Miquissone anataraji kuondoka mapema wiki ijao kuelekea Uturuki ambapo atajiunga na wenzie kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/2024

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER