Kikosi chetu kimeingia Fainali ya mlMichuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Azam FC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea leo Juni 26.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku matumizi makubwa ya nguvu yakitumika zaidi na kupunguza ladha kutokana na wachezaji kugongana na kuanguka mara kwa mara.
Hata hivyo, tulipiga krosi nyingi kipindi cha kwanza kutoka upande wa kulia zilizopigwa na Shomari Kapombe lakini hata hivyo ziliishia mikononi mwa mlinda mlango wa Azam, Mathias Kigonya.
Luis Miquissone alitufungia bao hilo pekee dakika ya 88 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bernard Morrison aliyeanzisha mpira haraka huku wachezaji wa Azam wakishangaa.
Ushindi huu unatufanya kukutana na watani wetu wa jadi Yanga kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa Julai, 25 katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Kocha Didier Gomes aliwatoa Mzamiru Yassin, Rally Bwalya na Clatous Chama kuwaingiza Medie Kagere, Morrison na Erasto Nyoni.
One Response
Nataka kuwa mwanachama wa simba nawezaje kujiunga nipo mkoani Njombe