Miquissone achomoa dakika ya mwisho

Bao la dakika ya mwisho lililofungwa na Luis Miquissone limetupa sare dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo mkali uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo Machi 10.

Kabla ya bao hilo tulifanya mashambulizi mengi langoni mwa Prisons lakini tulishindwa kuyatumia na kusababisha kupata sare.

Dakika ya 28 Chris Mugalu alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Prisons, Vedastus Mwihambi kuunawa mpira ndani ya 18.

Mwamuzi Emmanuel Mwandemba alimtoa kwa kadi nyekundu kiungo Jumanne Elfadhili baada ya kumchezea rafu Mzamiru Yassin.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Mzamiru Yassin, Perfect Chikwende na Rally Bwalya nafasi zao zikachukuliwa na John Bocco, Clatous Chama na Mzamiru Yassin.

Matokeo yametufanya kufikisha alama 46 tukibaki nafasi ya pili kwenye msimamo huku tukiwa na mchezo miwili mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER