Mikael Igendia Meneja mpya wa timu

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumuajiri Mikael Igendia raia wa Kenya kuwa Meneja wa timu na Mkuu wa Sayansi ya Michezo kwa mkataba wa miaka miwili.

Igendia (36) anachukua nafasi ya Patrick Rweyemamu ambaye amekuwa Mkuu wa Programu za soka la vijana.

Ujio wa Igendia unaongeza ufanisi katika benchi la ufundi kwakuwa yupo vizuri pia kwenye utimamu wa mwili pamoja na utawala wa timu.

Igendia amewahi kufanya kazi na Gormahia FC, timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Uwepo Igendia kwenye kikosi ni sehemu ya kuliboresha benchi letu la ufundi kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023/24.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER