Mhilu, Mkude kuanza dhidi ya Namungo

Winga Yusuph Mhilu na kiungo mkabaji Jonas Mkude wamepangwa kuanza katika mchezo wa wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC utakaopigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mara ya mwisho Mkude kuanza kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya kimashindano ilikuwa Mei 15 dhidi ya Kaizer Chiefs na mechi iliyopita dhidi ya Coastal aliingia kipindi cha pili na kuonyesha uwezo mkubwa.

Kocha Thierry Hitimana ameendelea kutumia washambuliaji wawili akimuanzisha Nahodha John Bocco na Kibu Denis.

Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Yusuph Mhilu (27), Rally Bwalya (8) John Bocco (22), Kibu Denis (38) Bernard Morrison (3)

Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Pascal Wawa (6), Abdulswamad Ally (25), Hassan Dilunga (24), Peter Banda (11), Medie Kagere (14), Ibrahim Ajibu (10), Duncan Nyoni (23).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER