Mgunda: Ya Kagera yamepita tunaganga yajayo

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema mchezo dhidi ya Kagera Sugar umepita sasa tunajipanga kwa mechi iliyo mbele yetu.

Mgunda amesema baada ya leo tuna siku tatu za kujiandaa na mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya KMC hivyo tunawekeza nguvu zetu huko.

Mgunda ameongeza kuwa katika mchezo dhidi Kagera kuna mapungufu yaliyojitokeza ambayo tutayafanyia kazi mazoezini na yale mazuri yataboreshwa ili tufanye vema mechi inayofuata

“Mchezo wa Kagera umemalizika, tumepambana kutafuta alama tatu lakini Mungu ametupa moja tunashukuru, tunarudi mazoezini kujiandaa na KMC.

“Tutakuwa na siku tatu ya kujiandaa kabla ya kucheza mechi yetu dhidi ya KMC yale mapungufu yaliyojitokeza tutayafanyia kazi kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER