Mgunda: Wachezaji walifuata maelekezo tuliyowapa

Kocha Mkuu Juma Mgunda ameweka wazi kuwa ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya KMC katika Uwanja wa CCM Kirumba umetokana na wachezaji kufuata maelekezo waliyowapewa.

Mgunda amesema tulikuwa tunajua tunaenda kukutana na timu yenye wachezaji bora hivyo tulipaswa kuhakikisha tunabana mianya yao na kutumia vizuri nafasi tutakazopata.

Mgunda ameongeza kuwa licha ya ushindi huo mnono lakini KMC ni timu nzuri na imetupa ushindani mkubwa jambo jema nikuwa tumepata pointi tatu.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kufuata maelekezo na mafunzo tuliyowapa na walipambana hadi mwisho kupigania pointi tatu, KMC ni timu nzuri na nilisema kabla ya mechi lakini tumefanikiwa kupata ushindi,” amesema Mgunda.

Kikosi kinarejea jijini Dar es Salaam kikiwa kimefanikiwa kupata alama saba kati ya tisa za Kanda ya Ziwa tulizocheza.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER