Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema ushindi mnono wa mabao 3-0 tuliopata dhidi Azam FC umetuongezea morali kuelekea kumaliza msimu.
Mgunda amesema ushindi huo ni jambo zuri kwa wachezaji kwakuwa imewaongezea morali na hali ya kujiamini.
Mgunda amesema haikuwa rahisi kupata ushindi huo mnono lakini tuliwasoma Azam na kufanikiwa kutumia mapungufu yao ambayo yametupa ushindi.
“Ni ushindi muhimu sana kwetu, tulihitaji kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kumaliza kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo.”
“Mchezo dhidi ya Azam umeisha sasa tunajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata, malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi iliyobaki,” amesema Mgunda.