Mgunda: Tupo tayari kwa Azam Kesho

Kocha msaidizi, Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC utakaopigiwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona kesho saa 9:30 Alasiri yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani.

Mgunda ameongeza kuwa mchezo wa kesho ni wa mtoano hivyo lazima mbinu zake ziwe tofauti na ilivyokuwa kwenye ligi.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, wachezaji wapo kwenye hali nzuri. Tunajua utakuwa mchezo mgumu, Azam ni timu nzuri na tunaiheshimu.

“Katika mechi za ligi msimu huu wamefanya vizuri dhidi yetu lakini mchezo wa kesho ni tofauti na mtoano kwahiyo hata mbinu zitakuwa tofauti, tumejipanga kwa ajili ya kupata ushindi,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kwa hali ilivyo kwenye michuano ya Azam Sports ndipo kuna matumaini ya kupata ubingwa zaidi ya ligi kwahiyo mchezo wa kesho tunahitaji kupata ushindi.

“Matumaini yetu yamebaki zaidi kwenye michuano hii, tunajua ugumu na umuhimu wa mchezo lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER