Mgunda: Tunaelekeza nguvu zetu Angola

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji tuliopata jana sasa tunaelekeza nguvu katika mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto
ya Angola ugenini.

Kauli hiyo imetolewa na kocha mkuu, Juma Mgunda ambapo amesema maandalizi dhidi ya De Agosto yameanza mara moja kabla ya kikosi kupaa kuelekea Angola.

Mgunda ameongeza kuwa mapungufu yaliyoonekana kwenye mchezo wa jana yatafanyiwa kazi mazoezini kabla ya kukutana na De Agosto mwishoni mwa juma lijalo.

“Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi mnono kabla ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa, utatuongezea morali katika mechi yetu ya ugenini nchini Angola.

“Maandalizi ya mchezo huo tayari yameanza na kitu kizuri hatutakuwa na mchezo wa ligi hivyo tutapata muda wa kufanya marekebisho yaliyojitokeza mazoezini,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER