Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema Coastal ni timu nzuri na inacheza pamoja lakini tuliwazidi uzoefu na ndiyo sababu ya kufanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini.
Mgunda amesema anawafahamu vizuri wachezaji wa Coastal na ameshiriki kuwajenga na tulitegemea kupata upinzani lakini jambo zuri tumepata pointi tatu muhimu ugenini.
Mgunda ameongeza kuwa mchezo ulikuwa mgumu na kipindi cha pili ilibidi tuongeze uzoefu na ndipo tulipofanikiwa kupata ushindi huo.
“Coastal ni timu nzuri, na wachezaji wengi nawafahamu na nilishiriki kuwajenga, tulijua tutapata upinzani mkubwa kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza lakini tuliwazidi uzoefu,” amesema Mgunda.