Mgunda: Tuliwasoma vizuri Big Bullets

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika nchini Mbalawi dhidi ya Nyasa Big Bullets tulirudi mazoezini na kuangalia ubora na mapungufu yao ambayo yametusaidia kuibuka kidedea.

Mgunda amesema baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini tulijua Bullets watakuja kushambulia kuanzia mwanzo kwa kuwa watakuwa hawana cha kupoteza ndiyo maana na sisi tulijipanga kwa hilo.

Mgunda amesema pamoja na ushindi tuliopata ugenini tulijua bado mechi haikuisha na tulihitaji kupata mabao zaidi ili kujihakikishia kusonga mbele.

“Kama nilivyosema wiki iliyopita mechi ilikuwa haijaisha. Tulijua Big Bullets watakuja kutushambulia kwa kuwa hawana cha kupoteza hivyo tulijiandaa kuwadhibiti na kuhakikisha tunatumia nafasi tunazopata.

“Nawapongeza wachezaji kwa kufuata maelekezo tuliyowapa, wamepambana mpaka mwisho kuwapa furaha Wanasimba,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER