Mgunda: Tulitegemea Ushindani mkubwa kutoka kwa Coastal

Kocha Msaidizi, Juma Mgunda amesema kabla ya mchezo wetu wa hatua ya tatu ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Coastal Union tulitegemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa ‘Wagosi hao’ na ndicho kilichokea uwanjani.

Mgunda amesema katika mechi yoyote ya hatua ya mtoano inakuwa ngumu kwakuwa hakutafutwi alama bali ushindi hivyo mbinu ndizo zinaamua.

“Tulitegemea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Coastal nasi tulijipanga kwa hilo, wachezaji walihakikisha wanafuata vizuri maelekezo tuliyowapa,” amesema Mgunda.

Akizungumzia kuhusu mchezo wa hatua ya 16 bora ambao tutakutana na African Sports pia kutoka Tanga, Mgunda amesema.

“Pia itakuwa mechi ngumu, kama nilivyosema lakini kila mchezo una mipango yake na muda ukifika tutajipanga kwa mechi hiyo.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda taji hili na ili tufanikiwe tunapaswa kushinda kila mchezo kwakuwa huku hakutafutwi alama bali ushindi,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER