Mgunda: Tulipambana

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema wachezaji walipambana wakati wote wa mchezo dhidi ya watani wetu Yanga lakini hatukufanikiwa kupata alama tatu.

Mgunda amesema wachezaji walicheza vizuri na walijitoa mpaka tone la mwisho la jasho lakini siku zote mpira una matokeo matatu, tumepata alama moja tunajipanga kwa mchezo ujao.

Mgunda ameongeza kuwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo tutayafanyia kazi mazoezini na mazuri tutayaboresha ili mechi ijayo tupate alama tatu.

“Wachezaji wamepambana muda wote, lengo lilikuwa ni kupata pointi tatu lakini haikuwa hivyo. Tuliingia kwa kujua utakuwa mchezo mgumu na tulijitahidi kuwadhibiti wapinzani.

“Katika mchezo wa leo kulikuwa na mazuri ambayo tutayaboresha ili tufanye vizuri mechi inayofuata na yale mapungufu tutayafanyia kazi mazoezini,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER