Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema Eagle FC tulikuwa hatuijui na hatukuwahi kuiona ikicheza ndiyo maana tulianza na sehemu kubwa ya kikosi kilichozoeleka.
Mgunda amesema ni vigumu kucheza na timu ambayo huifahamu ubora wake wala mapungufu ndiyo maana tulipanga kikosi kamili na baadaye kuingiza wale ambao hawakupata nafasi sana.
Mbali na ushindi wa mabao 8-0 tuliopata Kocha Mgunda amesema Eagle ina wachezaji wenye vipaji vikubwa na anaamini katika siku za usoni watafanya makubwa.
“Tulikuwa tunacheza na timu ambayo hatuijui ndiyo maana tulipanga kikosi kamili ili tuwafahamu ubora na mapungufu yao na ndicho kilichotusaidia kupata ushindi.
“Eagle pamoja na kupoteza lakini wachezaji wake wana vipaji vikubwa, naamini watafanya vizuri siku za usoni,” amesema Mgunda.
Mgunda ameongeza kuwa mchezo wa jana ni maandalizi kuelekea mzunguko wa pili wa ligi ambao utaanza siku chache zijazo.