Mgunda: Tuko timamu kwa Azam kesho

 

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC yamekamilika na wachezaji wako kwenye hali nzuri kupigania alama tatu.

Mgunda amesema mchezo utakuwa mgumu sababu unakutanisha timu bora na tumechukua tahadhari zote kwa kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunachukua pointi zote.

Mgunda ameongeza kuwa katika mchezo wa kesho tutawakosa wachezaji Sadio Kanoute, Israel Patrick na Jimmyson Mwanuke ambao ni majeruhi wakati Mzamiru Yassin anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tunajua itakuwa mechi ngumu, tunaiheshimu Azam ni timu bora lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho,” amesema Mgunda.

Kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kushoto Gadiel Michael amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji na wao wako tayari kupambana na kuwapa furaha.

“Sisi wachezaji tuko tayari, makocha wametuelekeza mazoezini kazi yetu ni kwenda kutekeleza uwanjani, kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema Gadiel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER