Mgunda: Tuko tayari kwa Mtibwa kesho

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mgunda amesema Mtibwa ni timu nzuri na ipo kwenye kiwango bora kwa sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunapambana kupata alama zote tatu.

Akizungumzia hali za wachezaji Mgunda amesema jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba idadi ya majeruhi imeendelea kupungua na waliobaki ni wawili; Jimmyson Mwanuke na Nelson Okwa.

Aidha Mgunda amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji na kusahau matokeo ya mchezo uliopita kwa kuwa hali hii ni kawaida.

“Kikosi kipo tayari kwa mchezo wa kesho, tunaiheshimu Mtibwa ni timu nzuri ina wachezaji wazuri na ipo kwenye kiwango bora kwa sasa lakini tumejiandaa kupambana kupata ushindi,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER