Mgunda: Tuko tayari kwa Kagera kesho

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kesho saa moja usiku katika Uwanja wa Kaitaba yamekamilika na tuko tayari kwa mpambano.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na hakuna yeyote atakayekosekana kutokana na kupata majeraha au sababu nyingine, hivyo atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

Mgunda ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Kagera lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuondoka na alama zote tatu.

“Tunamshukuru Mungu tumefika salama hapa Kagera, maandalizi yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tupo tayari kwa mchezo,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake kiungo, Nassor Kapama amesema wao kama wachezaji wanafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunawaheshimu Kagera lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata alama zote tatu.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Kagera ni timu nzuri na ipo nyumbani lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda,” amesema Kapama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER