Mgunda: Tuko tayari kwa Derby

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa Derby dhidi ya Yanga yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema utakuwa mchezo mgumu wa ushindani lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda na kuchukua alama tatu muhimu.

Mgunda ameongeza kuwa katika mchezo huo tutaendelea kuwakosa Shomari Kapombe na Jimmyson Mwanuke ambao wanaendelea kuuguza majeraha yao.

“Mchezo utakuwa mgumu, lakini sisi tumejiandaa kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu huku tukicheza aina yetu ya mpira tulioizoea. Mechi ya Derby ni ngumu lakini tuko tayari,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kwa upande wao wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu kuhakikisha tunapata ushindi.

Zimbwe amesema wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo na wamejipanga kuhakikisha wanawapa furaha Wanasimba kesho.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kwa mchezo, tunahitaji alama tatu kwa ajili ya kujiimarisha kileleni pia tuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER