Mgunda: Sare ni sehemu ya mpira

Kocha Mkuu Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa kutoka sare ni sehemu ya mpira na hawezi kumtupia lawama mchezaji mmoja mmoja.

Mgunda amekiri kuwa safu yetu ya ulinzi ilishindwa kutimiza majukumu yake vizuri na kuruhusu Mbeya City kupata bao rahisi la kusawazisha lakini ndiyo sehemu ya mpira huwezi kufanya kila kitu kwa usahihi ndani ya dakika 90.

Mgunda ameongeza kuwa hakuna mchezaji ambaye anapenda kufungisha ili timu yake kupoteza au kupata sare kinachotokea ni sehemu ya mchezo.

“Kwanza lazima tukubaliane kutoa sare kwenye mpira si dhambi, niwapongeze Mbeya City kwa kucheza vizuri na kutumia udhaifu wetu kupata bao la kusawazisha, sisi tunarudi mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata.

“Matokeo haya bado hayajatukatisha tamaa tutaendelea kupambana hadi mwisho kupigania ubingwa,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER