Mgunda: Nawapongeza wachezaji wangu

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya na kufanikisha kupata ushindi wa bao moja dhidi ya Ihefu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mgunda amesema haikuwa mechi rahisi ingawa wengi wanadhani Ihefu ni timu dhaifu lakini walitupa upinzani mkubwa na walicheza kwa mfumo wao waliojiwekea.

Mgunda ameongeza kuwa ligi ni ngumu na ratiba imebana kutokana na mechi kuwa karibu karibu lakini wachezaji wanapambana kuhakikisha tunashinda bila kujali nini ndiyo maana tunapaswa kuwasapoti.

Mgunda pia amesisitiza mshikamano baina ya timu na mashabiki unatakiwa kuendelea kwa kuwa tunacheza kila baada ya siku mbili au tatu.

“Kwanza niwapongeze wachezaji kwa jinsi wanavyojitoa, haikuwa mechi rahisi Ihefu ni timu nzuri na ilicheza kwa mipango muda wote kikubwa tumepata pointi tatu tunajipanga kwa mchezo unaofuata.

“Nasisitiza mshikamano baina yetu, ligi ni ngumu na ratiba imebana, wanasema ndege wafananao huruka pamoja hata sisi tunapaswa kuwa hivyo,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER