Licha ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 kocha Juma Mgunda ameisifu Geita Gold na kusema ni timu nzuri na imetupa ushindani mkubwa.
Mgunda amesema mpira ni mchezo wa makosa ambapo wenzetu waliyofanya nasi tukayatumia vizuri kupata ushindi mnono.
Mgunda ameongeza kuwa tangu tunatoka Dar es Salaam kuja Mwanza tulikuwa tunajua tunaenda kukutana na timu imara na tulijipanga kuwakabili.
“Kupata ushindi mabao matano haimaanishi Geita ni timu mbovu, bali mpira ni mchezo wa makosa wameyafanya tumeyatumia vizuri.
“Jambo jema tumepata alama tatu ugenini tunajipanga kwa mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar,” amesema Mgunda.