Mgunda: Mipango yetu ilikuwa bao la mapema tukafanikiwa

Kocha msaidizi, Juma Mgunda amesema katika mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga tulikuwa na lengo la kutafuta bao la mapema na tumefanikiwa katika hali hiyo.

Mgunda amesema baada ya kupata bao dakika ya pili tuliongeza kasi ya kutafuta jingine hali iliyowafanya wapinzani Yanga kutoka mchezoni.

Mgunda ameongeza kuwa baada ya kupata bao la kwanza tulipoteza nafasi nyingine mbili za haraka kupitia kwa Jean Baleke na ndicho kimechangia kupata matokeo chanya.

“Mpango wetu ulikuwa ni kupata bao la mepema, kocha mkuu Robertinho alituambia jana kabla ya mchezo tunahitaji kufanya hivyo.

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji wetu kwa kufuata maelekezo waliyowapa, haikuwa mechi rahisi lakini jambo bora tumefanikiwa kushinda na kupata pointi tatu muhimu,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER