Mgunda: Mchezo wa Al Hilal utakuwa kipimo kizuri kwetu

Kocha Msaidizi, Juma Mgunda amesema mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya Al Hilal utakuwa kipimo kizuri kwetu kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya itakayopigwa Februari 11.

Mgunda amesema Al Hilal ni moja ya timu bora barani Afrika ambapo itatupa mwanga wa hali ya ubora wa kikosi chetu kuelekea mchezo wa Horoya.

Mgunda ameongeza kuwa hata Al Hilal watapata maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns kwakuwa wanakutana na timu bora.

“Al Hilal ni timu nzuri barani Afrika, tunategemea itakuwa kipimo kizuri kwetu kuelekea mchezo dhidi ya Horoya.

“Tumetoka kucheza jana mechi ya ligi na kikosi kimefanya mazoezi leo tayari kwa kesho, niwatoe hofu Wanasimba kuwa tuna kikosi kipana na wachezaji ambao walikuwa majeruhi kwa muda mrefu tunategemea kuwatumia kesho,” amesema Magunda.

Kwa upande wake kocha wa Al Hilal, Florent Ibenge amesema mchezo wa kesho utakuwa ni kama wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwakuwa anaenda kukutana na timu bora zaidi.

Ibenge amesema anatamani Simba kuwa bora katika mchezo wa kesho ili apate kuona mapungufu ya kikosi chake kabla ya kukutana na Mamelodi.

“Mchezo wa kesho utakuwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, tunakutana na Simba timu imara zaidi. Itatupa mazoezi mazuri na kipimo.

“Tumekuwa na wiki nzuri ya maandalizi hapa Tanzania kabla ya kuelekea Afrika Kusini, ni matarajio yetu tutafanya vizuri,” amesema Ibenge.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER