Mgunda: Mchezo dhidi ya Polisi tumeupa umuhimu mkubwa

Kocha msaidizi, Juma Mgunda amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania tumeupa umuhimu sawa na mingine iliyopita na tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Mgunda amesema wengi wanadhani tutauchukulia kawaida kwakuwa hakuna kitachobadilika lakini hiyo ni tofauti kwetu kwasababu tunapaswa kushinda kila mchezo.

Mgunda ameongeza kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri kinachosubiriwa ni muda ufike tuingie uwanjani kupambania pointi tatu.

“Mchezo wa kesho ni muhimu kama ilivyo mechi nyingine, ingawa matokeo hayatabadili chochote kwetu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa kesho isipokuwa Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao wanatumikia adhabu. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Mgunda.

Mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania utapigwa kesho saa moja usiku katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER