Mgunda: Mchezo dhidi ya Mtibwa utakuwa na ushindani mkubwa

Kocha Msaidizi, Juma Mgunda ameweka wazi sababu zitajazoufanya mchezo wetu wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Manungu Complex saa 10 jioni kuwa wa ushindani.

Mgunda amezitaja sababu hizo kuwa ni kutokana na Mtibwa kuwa nyumbani, ligi kuelekea ukingoni na pia tuliwafunga kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hivyo wapambana na wao kutafuta pointi tatu.

Mgunda amesema kwa kulitambua hilo tumejipanga kuwakabili Mtibwa na lengo letu ni kuhakikisha tunapambana hadi mwisho kutafuta pointi tatu.

Kuhusu hali ya kikosi, Mgunda amesema wachezaji wote 25 tuliosafiri nao wapo kwenye hali tayari kwa mchezo hakuna yoyote ambaye tutamkosa kutokana na kupata majeruhi.

“Ligi inaelekea ukingoni na kila timu inajipanga kuhakikisha inapata pointi tatu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa lakini tumejipanga kupambana kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Nassor Kapama amesema tunaiheshimu Mtibwa na tunategemea mchezo mgumu lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo, Mtibwa ni timu nzuri na ina benchi zuri la ufundi tunaiheshimu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda, kikubwa mashabiki wetu tunawaomba mjitokeze kwa wingi,” amesema Kapama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER