Mgunda: Ligi ni ngumu

Kocha Mkuu Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa msimu huu ligi ni ngumu na kila timu bila kujali iko kwenye nafasi gani imejiandaa vizuri kupigania pointi tatu.

Akizungumzia mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC, Mgunda amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda ameongeza kuwa ukimtoa Peter Banda aliyepata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars, Israel Patrick na Jimmyson Mwanuke ambao ni majeruhi wa muda mrefu nyota wengine wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

Kuhusu suala la kutengeneza nafasi nyingi na kutumia chache kupata mabao Mgunda amesema; “ni kweli tunatengeneza nafasi nyingi lakini tunatumia chache, mimi na wasaidizi wangu tunaendelea kulifanyia kazi mazoezini kulipunguza kama si kuliondoa kabisa,”

Naye Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari asilimia 100 kuhakikisha wanapambana kupigania alama tatu katika uwanja wa nyumbani.

Zimbwe amesema ushindi kwenye mchezo wa kesho utatusaidia kupunguza tofauti iliyopo baina yetu na wanaongoza na kuzidi kuwapa presha.

“Sisi wachezaji tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua utakuwa mgumu. Tumetoka kucheza mechi ngumu dhidi ya Singida na hatujapata matokeo mazuri kwa hiyo tutajitahidi kupata ushindi kwenye mchezo wa nyumbani,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER