Mgunda: Derby itakuwa ngumu

Kocha Mkuu Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa mchezo wa Derby dhidi ya watani Yanga Jumapili hautabiriki utakuwa mgumu.

Mgunda amesema mchezo wa watani siku zote ni mgumu ndiyo maana anaendelea kukiandaa kikosi ambapo wachezaji wanajitahidi kufuata maelekezo yake mazoezini.

Ingawa itakuwa ni mchezo wake wa kwanza wa Derby, Mgunda amesema hana presha ya mechi ingawa anahafamu itakuwa ngumu na ya kuvutia kutokana na ubora wa timu zote kwa sasa.

“Mchezo utakuwa mgumu, siku zote mechi ya Derby haijawahi kuwa rahisi nasi tunajua, tunaendelea na mazoezi, nafurahi jinsi wachezaji wangu wanavyopokea maelekezo mazoezini.

“Ni kweli utakuwa mchezo wangu wa kwanza wa Derby lakini sina presha, najua itakuwa mechi nzuri kikubwa tuwaombee wachezaji waamke salama siku hiyo,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER