Mgunda, Chama wang’ara NBC Desemba

Kocha Juma Mgunda amechaguliwa kocha bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya NBC huku Kiungo Mshambuliaji Clatous Chama akichaguliwa mchezaji bora.

Kocha Mgunda ametuwezesha kushinda mechi nne na kutoka sare moja katika mwezi huo huku akiwapiku Nasreddine Al Nabi wa Yanga na Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars.

Kwa upande wake Chama amekuwa kwenye ubora na takwimu nzuri katika mwezi Desemba akicheza mechi tano sawa na dakika 450 akifunga mabao mawili na asisti tano.

Chama amewapiku Nahodha John Bocco na mshambuliaji Fiston Mayele ambao ameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

 

Takwimu za Mgunda za Desemba

Coastal Union 0-3 Simba

Geita Gold 0-5 Simba

Kagera Sugar 1-1 Simba

KMC 1-3 Simba

Simba 7-1 Tanzania Prisons

Mgunda ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo pia mwezi Novemba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER