Mgunda asisitiza mchezo wa kiungwana Zanzibar

Kuelekea mchezo wetu wa pili wa kirafiki tutakaocheza kesho dhidi ya Kipanga FC, Kocha Mkuu Juma Mgunda amesisitiza wachezaji wacheze kiungwana bila kuumizana.

Kauli hiyo ameitoa leo baada ya mchezo wa kwanza tuliocheza dhidi ya Malindi ambapo wachezaji walitumia nguvu ambazo zilikuwa zinahatarisha kazi zao.

Mgunda ameongeza kuwa kuumizana kwenye mpira inatokea lakini inakuwa ajali si kudhamiria na kuhatarisha maisha ya mwingine.

Akizungumzia mchezo wa kesho, Mgunda amewaomba mashabiki kuja kwa wingi Uwanja wa Amani kushuhudia burudani safi na soka la ushindani kutoka kwa timu zote.

“Nasisitiza tu wachezaji wote wacheze soka la kiungwana na ikitokea kuumizana iwe bahati mbaya si kudhamiria. Mpira ni kazi ambayo unahitaji utimamu wa mwili kwa hiyo ukimumuumiza mwenzio unaweza kumharibia maisha.”

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika kikubwa nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mechi naamini itakuwa nzuri ya kuvutia,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER