Mgunda afanya mabadiliko matatu dhidi ya Singida leo

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu kuelekea mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Uwanja wa Liti saa 10 jioni.

Mgunda amemuanzisha mlinda mlango Beno Kakolanya, kiungo mkabaji Sadio Kanoute na Kibu Denis ambao hawakuanza katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.

Moses Phiri ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji ambapo atasaidiwa na Kibu pamoja na Pape Sakho.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Kibu Denis (38), Moses Phiri (25), Mzamiru Yassin (19).

Wachezaji wa Akiba

Aishi Manula (28), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Peter Banda (11), Nassor Kapama (35), Habibu Kyombo (32).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER