Mgosi: Tupo tayari kwa mashindano ya U20

Kocha Mkuu wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Mussa Hassan Mgosi amesema maandalizi kuelekea michuano ya vijana ambayo itaanza leo yamekamilika.

Mgosi amesema kikosi chetu kimepata maandalizi yote na ameushukuru Uongozi pamoja na wadhamini MobiAd kuhakikisha kila kinachostahiki kinapatikana.

Mgosi ameongeza kuwa mara kadhaa tumekuwa tukiishia robo fainali na nusu lakini msimu huu tumejipanga kuhakikisha tunafika fainali na kuchukua ubingwa tukianza na mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar.

“Maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Kagera Sugar yamekamilika, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, malengo yetu ni kuhakikisha tunafika fainali na kuchukua ubingwa,” amesema Mgosi.

Kwa upande wake nahodha wa timu, Isack Emmanuel amesema kwa upande wao kama wachezaji wapo tayari kuipigania timu kupata ushindi katika kila mchezo mpaka tuchukue ubingwa.

“Sisi tunataka ubingwa, halafu pia kama wachezaji tunataka kufanya vizuri ili kuonyesha vipaji vyetu ikiwezekana tupandishwe kwenye timu ya wakubwa,” amesema Isack.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER