Mgosi: Tunautaka Ubingwa TWPL

Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi amesema malengo ya timu hiyo ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) msimu huu.

Mgosi ameyasema hayo wakati wa akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho wa Derby dhidi ya Yanga Princess.

Mgosi amesema mchezo huo utakuwa mgumu na Simba na Yanga wanapokutana lazima mchezo uwe mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

“Itakuwa mechi ngumu, hii ni Derby lazima iwe mechi ngumu lakini kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, malengo yetu ni kuchukua ubingwa,” amesema kocha Mgosi.

Kwa upande wake nahodha wa Queens, Violeth Nicholas amesema wao kama wachezaji wapo tayari kuikabili Yanga na wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo la kutafuta ushindi.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua utakuwa mchezo mgumu Yanga ni timu bora lakini sisi tupo vizuri na tunaamini tutaibuka na ushindi,” amesema Violeth.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER