Mgosi: Kikosi kipo kamili kuimaliza Yanga Princess Kesho

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Mussa Mgosi amesema kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women Premier League) dhidi ya watani wa jadi Yanga kikosi chake kiko vizuri na hakuna mchezaji yeyote majeruhi.

Mgosi amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na huku akisisitiza kila kitu kiko sawa na kinachosubiriwa ni kesho tu dimbani.

Nahodha huyo wa zamani wa Simba SC, ameongeza kuwa hafuti kauli yake ya kuwa hatofungwa mechi yoyote dhidi ya Yanga kwa muda wote atakaokuwa kocha wa timu hiyo.

“Mechi itakuwa nzuri na ngumu lakini kesho ndiyo siku Yanga Princess itakapokaa kwenye nafasi yake. Lengo letu ni kuchukua ubingwa mara ya pili mfululizo,” amesema Mgosi.

Kwa upande wake Nahodha, Mwanahamisi Omary amesema anajua Yanga ina kikosi kizuri msimu huu lakini hakuna njia yoyote itawafanya kuepuka kipigo kutoka kwetu kesho.

“Tuko tayari kwa ajili ya mchezo kesho, mimi kama nahodha pamoja na wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na tunamuomba Mungu tuamke salama na matumaini ya kuibuka ushindi ni makubwa,” amesema Mwanahamisi.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER