Meya wa Kizicahamam aitembelea timu Uturuki

Mstahiki Meya wa Jimbo la Kizicahamam lililopo hapa Ankara Uturuki, Suleyman Acar aimetembelea timu yetu na kusalimiana na benchi la ufundi na wachezaji leo jioni.

Meya, Acar amepokelewa na Meneja wa timu, Mikael Igendia kisha akatambulishwa kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Baada ya salamu nahodha, John Bocco amemkabidhi jezi yetu rangi nyekundu na kupiga picha ya pamoja na wachezaji kabla ya ratiba ya mazoezi kuendelea.

Meya, Acar amesema amefurahia ushirikiano na moja ya timu kubwa Afrika iliyokwenda nchini kwake kufanya maandalizi kwa ajili msimu mpya wa mashindano kutokana na kuamini kuna miundombinu mizuri.

“Simba inafaidika kwa kupata kila kitu wanachohitaji hapa, kuna hali ya hewa nzuri kwa timu kufanya maandaluizi ya msimu pamoja na viwanja.”

“Ushirikiano huu na Simba hautaishia hapa bali hata wakati mwingine mkihitaji kufika eneo hili tupo tayari kuwapatia kila kitu mnachohitaji kwa ubora wa hali ya juu,” amesema Meya Acar.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER